May 26, 2017

SIMU MPYA ZA NOKIA 3310 ZAINGIA SOKONI

Simu za Nokia 3310 zimeanza kuuzwa tena madukani, takriban miaka 17 baada ya simu hizo kuanza kuuzwa mara ya kwanza.
Simu za sasa zina kamera ya megapikseli mbili na zinategemea teknolojia ya 2.5G kumpa mteja huduma ya kiwango cha chini sana cha mtandao wa Intaneti.
Simu hiyo inauzwa £49.99 (Dola 65).

STAA WA FILAMU ZA NGONO ALIYEDAI KUPEWA UJAUZITO NA DRAKE AONESHA KITUMBO NA PICHA WAKIWA ‘DATE’

Staa wa picha za ngono, SophieBrussaux aliyedai kupewa ujauzito na Drake amejitokeza na kumwaga mchele zaidi. Mrembo huyo anadai kuwa Drizzy alimuambia aichomoe mimba yake lakini alikataa.

MAMBO 5 YATOKAYOKUACHA KINYWA WAZIMambo haya ni kustajabisha sana kama si kukustajabisha basi yatakuacha mdomo wazi,

KLABU YA EVERTON KUFANYA ZIARA NCHINI TANZANIA


Klabu ya soka ya Everton inayoshiriki Ligi kuu nchini Uingereza, inatarajia kufanya ziara nchini Tanzania mapema mwezi Julai mwaka huu kama sehemu ya maandalizi ya msimu ujao 2017/2018 na itacheza michezo kadhaa za kirafiki katika uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam.

VIDEO: KIJANA WA RWANDA ALIETAJIRIKA KUPITIA FACEBOOK

Wakati watu wengi hutumia mitandao ya kijamii kwa kupiga stori na jamaa na marafiki zao,wengine hujaribu bahati zao kimaisha kwa kutumia mitandao hiyo.

VIDEO: BELLE 9 & G NAKO - MA OLE

NJIWA ALIYETUMIKA KUSAFIRISHA DAWA ZA KULEVYA, AKAMATWA

Polisi wa Kuwait wamemkamata njiwa aliyekuwa amebeba dawa za kulevya aina ya Ketamine ambaye alikuwa amenasa kwenye bati la jengo la forodha katika Bandari ya Abdel iliyopo mpakani mwa Kuwait na Iraq.

May 25, 2017

MUME WA ZAMANI WA ZARI (IVAN) AFARIKI DUNIA

Aliyekuwa mume wa Zarinah Hassan ‘Zari The Boss Lady’ na mzazi mwenzake ‘Ivan Ssemwanga’ amefariki dunia baada ya kuugua kwa muda kiasi cha kulazwa katika hospitali ya Steve Biko Academic mjini Pretoria nchini Afrika Kusini.

Ivan alipimwa na kuonekana kuwa na kiharusi hata kukosa fahamu kwa muda wa siku 11 ambapo taarifa za awali zilisema kuwa alisumbuliwa na maradhi ya Shambulio la Moyo (Coronary Artery Disease). Wiki iliyopita alikimbizwa hospitali mara tu baada ya kupoteza fahamu hali ambayo ilionekana kumnyima raha Zari hata kutuma ujumbe katika mtandao wa SnapChat na Instagram kuwa yuko katika kipindi kigumu hivyo wamuombee Ivan kutokana na hali aliyokuwa nayo kiafya kuonekana kuwa mbaya.
Kupitia ukurasa wa Instagram Zari ametuma ujumbe wa taarifa za kufariki kwa mzazi mwenzake huyo,Hata hivyo Zari na Ivan amefanikiwa kupata watoto watatu ambao Zari anaishi nao Afrika Kusini.
"Rest in Peace"


VIDEO:SINA VITA NA MTANDAO WOWOTE WA KUUZA NYIMBO - DIAMOND PLATNUMZ

Tangu Diamond Platnumz azindue mtandao wake wa kuuza nyimbo online (Wasafi.Com) kitaani kumekuwa na story kuwa Diamond hana maelewano mazuri na mitandao mingine ya kuuza ngoma online.
Diamond Platnumz afunguka.

NEW VIDEO: LAVALAVA - TUACHANE

May 24, 2017

VIDEO: NILICHOKILENGA KIMEFANIKIWA - BEN POL

Siku chache zilizopita moja kati ya story kubwa mitandaoni ilikuwa ni kuhusu picha alizokuwa akizipost msanii wa Bongo Fleva Benpol, picha ambazo zilikuwa zikimuonyesha akiwa mtupu na amefungwa kamba kama vile ametekwa.

VIDEO: KHALIGRAPH JONES X RAYVANNY - CHALI YA GETTO

KAMA HUJUI KUANDIKA NYIMBO WCB HUPATI NAFASI – DIAMOND

Rais wa lebo ya WCB Diamond Platnumz amefunguka na kusema ni vigumu kwa msanii kujiunga na lebo yake hiyo kama hajui kuandika nyimbo.
Diamond amekiambia kipindi cha XXL cha Clouds Fm kuwa wimbo unapoandikwa ndani ya lebo hiyo mara zote unakaguliwa na watu wote ili kubaini kama kuna makosa na kuelekezana.
Kwanza Rich Mavoko ndiye mgumu kwenye kupitisha nyimbo, ikitoka hapo Ravvanny aipitishe, Queen Darleen aipitishe, ikitoka hapo niipitishe mimi, iende kwa Mkubwa Fella na Babu Tale waipitishe na Sallam aipitishe, ukitoka hapo wewe ni mwanaume haswa,” amesema Rich Mavoko na kuongeza.
Kwa hiyo wengi wanakuwa na uwezo mkubwa. Labda unaweza ukaja ukasikia kitu kidogo, ukasema ukiweka hapa kitu flani itakuwa poa zaidi, yaani ukiandika unaandika haswa,” ameeleza Diamond.

VIDEO: JOHN LEGEND - SUREFIRE

BARAKA THE PRINCE AMPONDA BEN POL

Baada ya Mwimbaji Ben Pol kuachia wimbo wake mpya aliomshirikisha Darassa, wimbo ambao alianza ku-promote ujio wake kwa kupost picha akiwa bila nguo, kumekua na mapokezi ya tofautitofauti kutoka kwa watu mbalimbali kutokana na picha hizo alizozitanguliza.

May 23, 2017

U HEARD: DIAMOND BAADA YA KUDAIWA KUSHTUKA ZARI ALIPOENDA KUMUONA IVAN

May 22, 2017 kupitia U-heard ya XXL ya Clouds FM mtangazaji Soudy Brown ametusogezea story inayomuhusu mzazi-mwenza wa Zari,  Diamond Platnumz juu ya mama watoto wake huyo kwenda Hospitali kumjulia hali mume wake wa zamani Ivan.

May 22, 2017

MAMBO 8 YA KUSHANGAZA YANAYOFANYWA NA MWILI WAKO KUKULINDA PASIPO WEWE KUJUA

Mwili wa binadamu unafanya mambo mengi ya kibaiolojia ambayo mara nyingi ni vigumu kuyaelewa.

Mwili una mifumo mbalimbali ya ulinzi ambayo inatulinda na hatari zinazoweza kutudhuru. Mifumo hiyo inatulinda masaa 24 ya siku, Siku zote 7 za wiki, katika mambo yote yanayoweza kuhatarisha maisha yetu.

DRAKE ALIVYOVUNJA REKODI YA BILLBOARD KWA KUSHINDA TUZO 13

Drake amefanikiwa kushinda tuzo 13 kwenye usiku wa Billboard Music Awards 2017 na kufunika rekodi ya tuzo 12 alizowahi kushinda Adele kutoka Uingereza.

BASATA LALAANI PICHA ZA BEN POL, ‘TUTAZUNGUMZA NAYE KUJUA KAMA ANA TATIZO LA AKILI’

Katibu Mtendaji wa Baraza la Sanaa Tanzania, BASATA, Godfrey Mngereza amelaani picha ya utupu ya msanii wa R&B, Ben Pol ambayo imezua tafrani kubwa kwenye mitandao ya kijamii. Akizungumza na Dizzim Online, Mngereza amesema sanaa ya Tanzania bado haijafikia zama za kufanyika kitendo kama hicho na kwamba BASATA linakilaani.

BEN POL APIGA PICHA AKIWA MTUPU

Moja ya picha zilizopata comments nyingi Instagram siku mbili hizi ni picha za mwimbaji wa RNB Tanzania Ben Pol ambazo zilimuonyesha akiwa hajavaa nguo.